|
Ligi kuu soka Tanzania Bara yafika ukingoni jana
2009-04-27 12:26:56
By ITV Habari
Wakati ligi kuu soka Tanzania Bara ikifikia ukingoni jana hafla ya kukabidhiwa kombe kwa mabingwa wapya Dar es Salaam Young Africans imeingia dosari baada ya pambano lake dhidi ya Villa Sqaud kutochezwa kutokana na uwanja wa Uhuru kujaa maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam .
Mkuu wa kituo cha Dar es Salaam Msafiri Mgoi amesema baada ya makamisaa, msimamizi wa kituo na waamuzi kukagua uwanja huo imeonekana kwamba mchezo haungeweza kufanyika ambapo mchezo huo sasa umepangwa kufanyika leo.
|